Na. Rachael Mushala Disemba 2011, Bwana aliturudisha Kwake mimi na ndugu zangu. Ingawa baba yetu ni mchungaji, sisi wote tulikuwa tumerudi nyuma na kumuacha Bwana. Tulijifanya Wakristo mbele ya wazazi wetu na kanisa, lakini tuliishi maisha ya dhambi shuleni na wakati walipokuwa mbali na nasi. Tulidanganya na kutenda tuliyopenda. Lakini Mungu alifanya muujiza. Dada zangu wawili, kaka na mimi tukatubu na kumgeukia Mungu tena. Tulipojitoa tena kwa Mungu, tuliamua kumtafuta kwa maombi mazito. Tulitaka tuwe na uzoefu wa nguvu zake. Tulihisi kwamba kama tutamtafuta kwa bidii, atatujibu na kusema na sisi pia. Tulitaka sana ubatizo wa Roho Mtakatifu. Siku moja tulipokuwa tukiomba, mdogo wangu, Lois, aliyekuwa na miaka 10 wakati huo, alisema anaona malaika! Uwepo wa Roho Mtakatifu ulijaza chumba na mdogo wangu mwingine Zipporah akaanza kunena kwa lugha! Ilikuwa ajabu lakini mimi nilihisi nimeachwa kwa sababu ingawa tulikuwa tukiomba, kaka yangu na mimi hatukubatizwa na Roho Mt...