Dhambi inasababisha kifo cha kiroho na kupelekea mwanadamu kutengana na Mungu kabisa.

ACHA KUTENDA DHAMBI NI MACHUKIZO KWA MUNGU

Kuendelea kutenda dhambi na kujifariji katika uovu unaoufanya, na kujiona mjanja; ni Ishara ya kwamba hujajua nini kimekuleta Duniani.  Ndio umezaliwa katika hali ya uovu lakini hujazaliwa uishi katika hali Hiyo YA uovu.

Tazama NEEMA ya MUNGU ilivyofunuliwa kwa ajili yako...

TITO_2:11-12
"11 Maana NEEMA ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;"

Katika ulimwengu huu tumezaliwa tuishi katika utauwa yaani UTAKATIFU, maisha yasiyo na mawaa Bali yenye ushirika mkuu na MUNGU wetu.

MUNGU kwa UPENDO wake mkuu aliamua kumtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipote Bali awe na uzima wa milele (YOHANA 3:16)

NA huyu MWANA ndiye aliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu Sote.

WATHESALONIKE 5:9-10
" 9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;
10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala."

MUNGU hajatuweka ili atuhukumu aetuletea ukombozi ulio katika Kristo YESU ambaye alikufa kwa ajili ya wanadamu wote na ndiye mwasisi na mwenye NEEMA mkononi make ili watu wote wamjie Mungu kwa yeye. Maana ndiye njia ya Kweli na uzima (YOHANA 14:6).......... MTU hawezi kumuona MUNGU asipopitia kwa YESU KRISTO, yaani usipomwamini YESU huna mbingu za kuingia labda utengenezewe mbingu za kuingia na viongozi wako wa  DINI.

Kaa ukijua hukumu inawakalia wote wasio mwamini Yesu .

 YOHANA_3:17-20
" 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.""

#Ndugu yangu kwa nini uikimbie Nuru na kutafuta hukumu? YESU alikufa msalabani kwa ajili yako na kwa kupigwa kwake sis tumepona kutoka katika dhambi na kila aina ya uovu unaoweza kutuzinga na shetani mwasisi wa uovu naye hawezi kutupata tena. (ISAYA 53:5).

YESU ANAKUITA NJOOO..........!!!
MATHAYO 11:28
" 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."

NJOO UPUMZISHWE MZIGO WA dhambi haijalishi ni nyingi kiasi gani, YESU alikufa kwa ajili yako..

ISAYA 1:18-19
" 18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;"

Ukiri wako wa kumkubali YESU ndio Sababishia wokovu uumbike ndani  yako.

Maana 
#WARUMI 10:9-10
 "9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

KAZI KWAKO MPENDWA............

          TAFAKARI CHUKUA HATUA 

MUNGU AKUBARIKI SANA........

By: Mwl George John
Facebook page: Gospel Ministry
EMAIL: georgejohn330@gmail.com
Blog: gospelministryj.blogspot.com

You tube account: GEORGE JOHN

Comments

Popular posts from this blog

USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU