UKIRI WAKO NDIO USHINDI WAKO K umwona Mungu akitenda katika maisha yako inategemea ni kwa namna gani na mtizamo gani ulionao juu ya neno la MUNGU. Je, unalichulia NENO la MUNGU kama ahadi tu zilizo andikwa kwenye kitabu (BIBLIA)? Au Kama NENO hai litokalo kinywani mwa MUNGU likiwa na nguvu zake kufanya matendo makuu maishani mwako? WAEBRANIA 4:12 “12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Neno la MUNGU siku zote ni jipya kila siku, lina nguvu na linatenda kazi kama enzi zile za zamani, halijawai pungua nguvu. MUNGU analitukuza NENO lake kuliko jina lake (ZABURI 138:2). Kazi ipo kwetu kulitendea kazi NENO kwa namna tunavyotaka iwe maishani mwetu. Na hii inafanyika kwa namna tunavyolikiri NENO la MUNGU katika maisha yetu ya kila siku. Kukiri kwako kun...