UKIRI WA NENO LA MUNGU
UKIRI WAKO NDIO USHINDI WAKO
K
|
umwona Mungu
akitenda katika maisha yako inategemea ni kwa namna gani na mtizamo gani
ulionao juu ya neno la MUNGU. Je, unalichulia NENO la MUNGU kama ahadi tu
zilizo andikwa kwenye kitabu (BIBLIA)? Au Kama NENO hai litokalo kinywani mwa
MUNGU likiwa na nguvu zake kufanya matendo makuu maishani mwako?
WAEBRANIA
4:12
“12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu,
tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata
kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li
jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Neno la MUNGU siku zote ni jipya kila siku,
lina nguvu na linatenda kazi kama enzi zile za zamani, halijawai pungua nguvu.
MUNGU analitukuza NENO lake kuliko jina lake (ZABURI 138:2).
Kazi ipo kwetu kulitendea kazi NENO kwa namna
tunavyotaka iwe maishani mwetu. Na hii inafanyika kwa namna tunavyolikiri NENO
la MUNGU katika maisha yetu ya kila siku. Kukiri kwako kunakutengenezea hamasa Fulani
na nguvu ya kipekee Moyoni mwako ya kuona kuwa mambo yananenda kukaa sawa
haijalishi ni hali gani unaipitia.
Kusikia, Kuamini, na Kukiri Neno la MUNGU
kutakufanya kuwa mtu wa kubadilisha hali na mazingira na si mazingira kukubadilisha
wewe. Tunamuona mwanadamu wa kwanza ADAM
alivyotambua kuwa kuna nguvu katika kutamka Neno, alianza kubadilisha
mazingira. Alianza kuwapa viumbe majina, kila mnyama wa kufugwa na ndege wa
Angani na kila mnyama wa polini wote walipewamajina (MWANZO 1:20)… Biblia haitwambii kuwa
Mungu alimwambia Adamu awape viumbe majina lakini Automatically Adam alianza kuwapa
viumbe majina.
Kuna nguvu ya kipekee katika kutamka na
kutabiri kwa kutumia vinywa vyetu. Ndo maana nipenda sana kusema “KUKIRI KWAKO
KATIKA IMANI NDIO USHINDI WAKO”
ISAYA
55:10-11
"10
Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko;
bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu,
na mtu alaye chakula;
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo
katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo
litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma."
BIBLIA inavyo vitabu 66 vilivyojaa sheria/maagizo, na ahadi za
MUNGU zilizo kuu. KAZI WETU KUTENDEA
KAZI NENO
IMANI na MATOKEO YA IMANI vinategemea namna kanuni
hii inavyofanyiwa kazi……………………………………….
KUSIKIA NENO LA MUNGU -àKUAMINI -àKUKIRI NA KUTENDEA
KAZI NENO
Kusikia kuwa YESU anaponya haitoshi tu kwako wewe kupata uponyaji.
Kuamini tu moyoni mwako kuwa YESU anaponya haitoshi tu kwako kupokea uzima
mpaka pale utakapochukua jukumu la kukiri kile NENO linamaanisha, pale
utakapotendea kazi NENO la MUNGU kile linachokuagiza au Kulitamka kama vile ni
lakwako.
Kwa mfano: NENO la MUNGU linasema
KUMBUKUMBU
LA TORATI 28
"13 BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia;
nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu
wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;"
Kuwa kichwa sio tu pale utakapoamini kuwa wewe
utakuwa kichwa bali ni pale utakapokiri kwa kinywa chako kuwa "Mimi ni kichwa
Na wala sio mkia, nitashinda katika kila jambo nifanyalo, nitapiga hatua kwa
sababu Mungu wangu ndiye anipaye kushinda; ninakataa kufeli. Na kufeli kuwa
mkia, kuchoka, kukata tamaa, kufadhaika, na kuugua hakuna nafasi kwangu”
Huo ni mfano wa ni kwa namna gani MTU anaweza
kukiri ahadi za Mungu Na kushuhudia matendo makuu ya MUNGU. Imani bila matendo
imekufa....
Imetupasa kulitendea kazi NENO la MUNGU, Kukiri
hasa kile MUNGU ametuahidi. Tusishikilie mabango yenye ahadi mioyoni mwetu,
Bali tuzikiri hizo ahadi Na kuzifanya na kuzifanya kuwa zetu.
Kuna vielelezo vingi vya kuthibitisha kuwa
KUKIRI na kufanya kile ulichoagizwa na Neno la MUNGU ndio muujiza mkuu wa
kumwona MUNGU akifanya kwa ajili Na kuyaona mambo yakitokea automatically kwa
sababu wewe unayo mamlaka kuu.
Mara nyingi tumekuwa watu wa kutumia vinywa Na
maneno yetu ndivyo sivyo, na kuliacha pembeni jukumu kubwa na lenye maana la
kuzikiri ahadi za Mungu kana kwamba ni zetu.
MITHALI
12:14
"14
Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake;Na atarudishiwa matendo ya mikono
yake."
Ukikitumia
kinywa chako hasa katika kikiri Na kulitendea kazi
NENO la
MUNGU Hakika lazima ule matunda ya midomo yako kwa sababu umejua kutuma kinywa vizuri
katika kujitabiria mema.
Iko mifano yakutosha katika kuthibitisha kwa
kina kile ambacho tunapaswa kukiri na kufanya kulingana na kile tunachoagizwa
na NENO la MUNGU.
Mfano mojawapo ni……………………. Wa kutoka kitabu
cha EZEKIELI
EZEKIELI
37:3-10
"3
Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana
MUNGU, wajua wewe.
4
Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu,
lisikieni neno la BWANA.
5
Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu,
nanyi mtaishi.
6
Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika
ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi
ndimi BWANA.
7
Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii,
palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa
ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.
8
Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi
ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake.
9
Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana
MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa
waliouawa, wapate kuishi.
10
Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa
miguu yao, jeshi kubwa mno."
Ezekieli
alipoulizwa kama mifupa inaweza kuwa hai hakushangaa maana alijua kuwa MUNGU
ndiye awezaye kufanya vitu kuwa hai kwahiyo hill halimshindi. Lakini kuamini
kuwa MUNGU anaweza kufanya hivo halikuifanya mifupa iweze kuwa Hai, isipokuwa
nni pale tu alipoamua kufanya kama alivyoagizwa Na Bwana MUNGU kutoa unabii juu
ya mifupa kuwa hai.
Nasi kwa
vinywa vyetu tunayo nafasi ya kutabiri au kutoa unabii juu ya maisha yetu Na
kujinenea mambo mwema kwa kuzikiri ahadi za MUNGU mwetu kwa sababu, ahadi zote
za MUNGU zimetimilika ndani ya Kristo.
WAKOLOSAI
1:19
"19
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;"
Nasi
kwa sababu ttumefananishwa Na Kristo mwenyewe basi Ahadi zote za MUNGU
zimetimilika ndani yetu kwa sababu Kristo anaishi ndani yetu.
Na sisi sio watu wa kawaida, ni watu wa Milki ya
MUNGU Ukuhani ufalme Na tupate kuzitangaza fadhiri za MUNGU, Na MUNGU mwenyewe
ajidhihirishwa kwa walimwengu kupitia sisi, kama alivyojidhihirisha kwa
wanadamu Kupitia Kristo YESU mwana wake.
SALA
BABA katika jina la YESU KRISTO aliye Hai, ninakushukuru
kwa jinsi ulivyonikirimia Ahadi kubwa mno, ninashukuru kwa sababu nimeumbwa kwa
mfano wako, na ndani yangu imo nguvu yako kwa sababu unaishi ndani yangu. Ninakiri
kuwa mimi ni mshindi kwa sababu Kristo YESU Bwana wetu ameushinda ulimwengu. Nimebarikiwa
na nitazidi kubarikiwa kwa sababu ahadi zako ni Kweli na Amina, wewe hubadiliki
na wala NENO lako halitokuja kutanguka. Ninakiri kuwa kwangu hakuna magonjwa,
hakuna kufeli, hakuna madhaifu wala mahangaiko. Kila ulichokwisha kuahidi
kwangu hakika kinaenda kutimia katika jina la YESU. Ninahitaji Neema yako
iendelee kuwa pamoja nami siku zote niyashuhudie matendo yako makuu maishani
mwangu. Ili watu wengine wajue hakika ya kuwa wewe ndiwe MUNGU pekee yako na
wala hakuna Mwingine. Sifa, utukufu, adhama, mamlaka na enzi vina wewe BABA wa
MBINGUNI.
BY: MWL. GEORGE JOHN
GOSPEL MINISTRY
(Turning souls to christ)
Comments
Post a Comment