USIKUBALI KUACHA KUSOMA USHUHUDA HUU MPAKA
MWISHO.
Na. Rachael
Mushala
Disemba 2011, Bwana aliturudisha Kwake mimi na
ndugu zangu. Ingawa baba yetu ni mchungaji, sisi wote tulikuwa tumerudi nyuma na
kumuacha Bwana. Tulijifanya Wakristo mbele ya wazazi wetu na kanisa, lakini
tuliishi maisha ya dhambi shuleni na wakati walipokuwa mbali na nasi.
Tulidanganya na kutenda tuliyopenda. Lakini Mungu alifanya muujiza. Dada zangu
wawili, kaka na mimi tukatubu na kumgeukia Mungu tena. Tulipojitoa tena kwa
Mungu, tuliamua kumtafuta kwa maombi mazito. Tulitaka tuwe na uzoefu wa nguvu
zake. Tulihisi kwamba kama tutamtafuta kwa bidii, atatujibu na kusema na sisi
pia. Tulitaka sana ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Siku moja tulipokuwa tukiomba, mdogo wangu,
Lois, aliyekuwa na miaka 10 wakati huo, alisema anaona malaika! Uwepo wa Roho Mtakatifu
ulijaza chumba na mdogo wangu mwingine Zipporah akaanza kunena kwa lugha!
Ilikuwa ajabu lakini mimi nilihisi nimeachwa kwa sababu ingawa tulikuwa tukiomba,
kaka yangu na mimi hatukubatizwa na Roho Mtakatifu usiku ule. Ilikuwa kama Mungu
yuko kimya kwetu. Nilimlilia Mungu, nikimuomba asinipite. Kisha akampa ujumbe dada
yangu Zipporah akisema, “Mwambie Inonge (jina langu jingine), Nasikia maombi yake.
Mwambie azidi kuomba na asikate tamaa.”
Kubatizwa na Roho
Mtakatifu
Baadaye tuliamua kuendelea na maombi ya siku tano ya kufunga
na kumtafuta Mungu.
Katika kipindi hicho, tulisoma Biblia, tuliimba sifa na
kuabudu, na kuomba pamoja, sisi wote wanne. Nilisoma mistari yote niliyoweza kuipata
inayozungumzia Mungu anavyojibu tukiomba. Nilisoma mistari yote inayozungumzia
kuhusu ubatizo wa Roho
Mtakatifu. Nilimuomba Mungu kwa ajili ya Roho Mtakatifu. Moyo
wangu ulikuwa wakati wote ukimlilia kwa ajili hiyo.
Lakini alikuwa kimya. Sikumpata hadi siku ya tano ya saumu yetu
ndipo ilitokea. Kama saa 9 hivi alasiri, tulishakata tamaa, na kudhani Mungu amekataa
kutujibu, ingawa awali tulipanga kufungua ifikapo saa 10 jioni ya siku hiyo. Tulimaliza
kuomba pamoja, lakini baadaye nikajisikia kuendelea na maombi, hivyo nikaenda
chumba kingine kuendelea na maombi. Nilipoomba na kumsihi Mungu anijaze sifa
kwa ajili yake, nikaanza kunena kwa lugha! Sikuamini! Alikuwa amejibu. Niliendelea
kumsifu kwa lugha muda mrefu na tukafungua dakika kadhaa baada ya saa 10 jioni.
Kutengwa na Ulimwengu
Baadaye usiku huo, nikaingia kuomba peke yangu. Nilikuwa
naomba kwa lugha wakati
Bwana alipoanza kusema nami. Alisema tunatakiwa kuwa mbali na
utumwa wa aina
yoyote, ikiwa ni pamoja na mazoea mabaya ya TV, kwa sababu
anataka awe wa kwanza
katika maisha yetu. Kisha akasema wakati wowote tunapomuita
kwa dhati , anasikia.
Nikaenda kuwapa ndugu zangu ujumbe huo (wazazi wangu walikuwa
wameenda nje ya mji wakati huo). Kisha tukaanza kuomba pamoja na Bwana akaanza
kutupa jumbe nyingine zaidi. Alianza kusema na mimi na dada yangu Zipporah.
Akasema, “Naja upesi, na nitakuja kama mwizi usiku, hivyo nitamjua ambaye kweli
ni Wangu. Watu hawajali tena mtu akiwaambia kwamba ninakuja, kwa sababu nimechukua
muda mrefu. Kuja kwangu hakutachelewa tena. Ninakuja upesi kuliko mnavyodhani,
lakini swali ni je mtakuwa tayari? Kwa sababu ninakuja tu kwa ajili ya watu
watakatifu, na kama unaishi maisha matakatifu nitakuchukua. Ninakuja tu kwa
ajili ya wale wanaoishi maisha matakatifu. Wakristo wengi hawatakuwa tayari nitakapokuja,
na watabaki.”
Akasema, “Kwa sasa mlango uko wazi lakini muda
si mrefu utafungwa. Ingia kabla mlango haujafungwa. Nakungojea (mwanadamu) nikiwa
nimefungua mikono yangu ya upendo.” Akasema, “Nilitoa uhai wangu kwa ajili
yenu, wanadamu kwasababu ya upendo Wangu kwenu. Humjui mbingu ni tukufu kiasi
gani. Akili zenu za kibinadamu ni ndogo sana kulielewa hili. Lakini niliacha
mbingu tukufu ili nitembee kwenye dunia hii chafu ya dhambi ili niwaokoe,
niwafie. Hamjui niliteseka kiasi gani kwa ajili yenu. Yalikuwa mateso makali kuliko
mnavyoona kwenye TV – mabaya kuliko wanavyoonyesha kwenye filamu yoyote. Hivyo ndivyo
nilivyowapenda. Niliacha kila kitu kwa ajili yenu. Mnanipenda kiasi hicho pia?
Mko tayari kutoa sadaka kila kitu kwa ajili yangu? Kwa vile hivyo ndivyo upendo
Wangu ulivyo mkuu kwenu. Niliacha kila kitu kwa ajili yenu.
Hamjui maumivu kiasi gani mnasababisha kwangu mnapoenda mbali
nami. Kama mngejua, hamngefanya hivyo.” Nilitambua maumivu aliyokuwa nayo
moyoni mwake aliposema hivi. Niliweza kuhisi maumivu ya Yesu. Bwana alituambia
kuna mambo tunatakiwa kuacha kwa ajili Yake. Alituambia tunatakiwa kuuacha
ulimwengu na kuishi kwa ajili ya utukufu Wake. Alisema, “Lazima mjitenge, kwa sababu
ninyi ni nuru ya ulimwengu. Nuru inawezaje kuitwa nuru, kama inafanana na giza?
Lazima muwe tofauti ili muwe nuru ya ulimwengu.”
Uasi na Manabii wa Uongo
Bwana Yesu alisema, “Uasi
umeenea duniani. Manabii wengi wa uongo wameenea ulimwenguni wakifundisha
mafundisho ya kuzimu na kupeleka roho nyingi kuzimu. Muwe waangalifu na
msifuate miujiza. Sikuwaonya katika Neno Langu kwamba manabii hawa wa uongo
watakuja? Na sasa wako hapa wakihubiri tu kuhusu utajiri na kamwe hawaihukumu
dhambi. Wahubiri wanachozungumzia sasa ni utajiri na fedha,
lakini fedha ina maana gani kama nafsi yako inaungua kuzimu?
Sikusema muuze vyote
mlivyo navyo na kuwapa masikini fedha na kisha mnifuate?
Fedha ni shina la uovu wote. Msivutiwe nayo. Imewashawishi wahubiri wengi.
Wanachojali tu ni kujaza mifuko yao na kujaza makanisa yao, lakini kamwe
hawahubiri toba. Najua kwamba mkiwa bado duniani mtahitaji fedha nami nitawapa
kiasi mnachohitaji. Hazina yenu iliyobaki itakuwa salama mbinguni. Utajiri wote
mnaoutamani utatunzwa mbinguni ambako nondo hawawezi kuharibu. Dunia hii
itaharibiwa kwa moto, na
hakuna kitakachobaki.” Alisema, “Moyo wangu unauma ninapoona roho
zinapelekwa kuzimu na manabii wa uongo. Wako wengi; wachungaji wachache sana
wanahubiri Neno Langu. Wachache sana wanahubiri toba. Haijalishi kama wana
wafuasi wengi au wanatenda miujiza. Hata shetani anaweza kutenda miujiza.
Msifuate miujiza. Ndio maana nilisema katika Neno Langu kwamba wengi watakuja
kwangu siku ya mwisho na kusema, ‘Tulifanya miujiza katika Jina Lako,’ lakini
nitajibu, ‘Siwajui’” Mungu Anasikia Maombi Yako Yesu pia alituambia kamwe
tusiogope kuomba kwa sababu hakuna jambo kubwa kwa Mungu. Alituambia tuwe
wajasiri kwamba tunapoomba Bwana anasikia. Wakati mwingine tunapoomba, shetani
atakuja na aina zote za uongo akisema, “Mungu hakusikii. Mungu hasikilizi maombi
yako.” Lakini msimsikilize. Wakati mwingine Mungu anaweza kuwa kimya, lakini
anasikia mnapoomba. Alituambia, “Mnapoomba, wakati fulani jibu linaweza kuja
maramoja, lakini wakati mwingine inaweza kuchukua muda kwa sababu Mungu anataka
muwe na subira na kumtumaini. Wakati wote jibu litakuja kwa sababu ni ahadi
Yangu kwamba yeyote
anayeomba hupokea.”
Hatari ya Ibada ya
Sanamu
Bwana alituambia hatari ya ibada ya sanamu. Mdogo wangu
alikuwa anasoma shule ya
Kikatoliki. Ni moja ya shule bora sana katika nchi yangu
lakini walilazimishwa kuabudu sanamu. Wote walitakiwa kushiriki misa na kusujudia
sanamu. Yesu alituambia kwamba kaka yangu anapaswa kuondoka shule hiyo na kutubu
kwa kuabudu sanamu. Kama unaabudu sanamu kwa namna yoyote, tafadhali tubu. Kama
hutafanya hivyo, utaenda kuzimu. Usipende au kutoa ibada yako kwa kitu chochote
zaidi ya Mungu. Hiyo ni sanamu. Bwana anataka awe wa kwanza katika maisha yako.
Pia alituambia kwamba mpinga Kristo yuko karibu na atadanganya wengi. Yesu
alisema mpinga Kristo atafanya mambo mengi ya kufuru lakini Bwana atamseta.
Alisema, “Mpinga Kristo tayari yuko hapa na watu wengi tayari wanamfuata.
Hawajui ni mpinga Kristo na mamilioni wanamfuata bila kujua. Atainuka mara,
lakini na Mimi pia naja upesi.”
Hubirini Waliopotea
Kisha Bwana akasema ni wajibu wa kila Mkristo kuwahubiri
waliopotea. Alisema wengi wamepotea na wanakwenda kwenye laana ya milele kuzimu
na ni wajibu wetu kuwaonya na kuwaacha wenyewe wafanye uamuzi wanataka kwenda
wapi. Bwana Yesu Kristo alisema tusimhukumu yeyote na tusiseme, Hata kama
tutawahubiri Injili hawawezi kamwe kutubu. Alisema, “Mnajuaje hawawezi kutubu?
Sio kazi yenu kuhukumu.” Yesu alituambia, “Lazima muwaonye watu watubu na
msiogope kumuonya yeyote kwa kuona kwamba atawachukia. Wengi watawachukia, hata
wengi katika familia zenu watawachukia, lakini lazima muwaonye. Msiogope
kupoteza upendo wa mtu yeyote, kwa sababu upendo Wangu utakuwa badala ya upendo
wote ambao wangewapa. Upendo wangu ni safi kuliko dhahabu.” “Kuzimu ni mahali
pabaya sana. Kama kweli unampenda mtu utapenda aumie sasa kwa maonyo yako na
kuepuka kuzimu. Usimhukumu yeyote. Mwamuzi (hakimu) ni mimi peke Yangu. Lazima
umuonye kila mtu ili afanye maamuzi yake mwenyewe. Waambie ukweli. Waonye, wanaoamini
watakuja kwangu na wasioamini watahukumiwa, wakati watakapojuta kuzimu milele.”
Waonye Wanadamu kuhusu Kuzimu Kisha Bwana alituambia kwamba
ni Yeye alimwonyesha Angelica Zambrano, mbinguni na kuzimu na kwamba ushuhuda
wake ni kweli. Alisema, “Watu wengi wanasema hakuna kuzimu kwa sababu Bwana ni
Mungu
wa rehema. Ni kweli kwamba Mungu ni wa rehema, lakini
anaadhibu wanaogeukia mbali Naye. Wanawezaje kuzungumzia hukumu Zangu, wakati
hata hawanijui? Hawajawahi kamwe kujua nguvu Zangu? Kuzimu kweli ipo na
unapaswa kuwaonya watu. Waache wafanye uamuzi wao wenyewe.” “Nimepeleka watu
wengi mbinguni na kuzimu na kuwarudisha ili watoe ushuhuda, lakini kwa nini
watu hawaamini? Kwa nini mnatilia mashaka shuhuda zangu? Kuzimu panatisha na
sitamani kwamba yeyote aende huko.” Bwana aliposema hivi, nikahisi maumivu
Yake, nikahisi maumivu ya moyo Wake kwa ajili ya kudanganywa kwa dunia, huruma
Yake kwa watu Wake wanaodanganywa na manabii wa uongo ambao wanazungumzia
utajiri tu. Mmoja wa rafiki zangu alifariki miezi michache iliyopita na Bwana
akaniambia yuko kuzimu. Aliishi maisha ya dhambi na sikujali kumshirikisha
Habari Njema. Iliniumiza sana kusikia hilo, nikamlilia Yesu anisamehe kwa kutomuonya
katika maisha yake ya dhambi. Bwana alisema, “Usiogope kumuonya yeyote.” Kama
una wapendwa wako wanaoishi katika dhambi, nakuambia ni bora uwaambie ukweli hata
kama watakuchukia kwa ajili hiyo. Utakuwa umewapa fursa wafanye uamuzi wao wenyewe.
Fanya hivyo kwa upendo na huruma ili wamgeukie Mungu. Vyombo vilivyo Tayari na
Vinavyotii Vinahitajika Bwana alituambia hajali kanisa ni kubwa au dogo kwa
sababu anachoheshimu ni Neno Lake, Anajali tu kuhusu Neno Lake. Alisema, “Naweza
kumtumia yeyote, hata jiwe. Ninachotaka ni moyo ulio tayari.” Alituambia,
“Niliahidi katika Neno Langu kwamba wote wanaoniamini watafanya mambo makubwa
kuliko niliyofanya. Neno Langu halibadiliki. Natafuta vyombo vya kutumia.
Ninachohitaji tu ni moyo ulio tayari na nitautumia.” Pia alitutahadharisha na
kiburi. “Ninapoanza kumtumia yeyote, mtu huyo kamwe asifikiri ni wa pekee sana.
Watu wote ni sawa Kwangu na ninatumia chombo chochote kilicho tayari. Kamwe
usijivune nisije nikakuseta.” Bwana akatuambia shetani hana nguvu mbele Yake,
ni kama mdudu tu. Ndio maana hatupaswi kumuogopa. Nguvu pekee aliyo nayo ni ile
tu aliyowahi kupewa. Ameruhusiwa kuwajaribu ili Bwana ajue nani ni wa Kwake hasa.
Kisha Bwana akanionyesha upanga na akasema tutamshinda adui kwa kutumia upanga
huo.
Ufunuo wa Kuzimu
Kwa wakati ule, hizi ni jumbe alizotupa kwa ajili ya
ulimwengu, lakini baadaye Septemba 2012
tukiwa kwenye maombi, Bwana alijidhihirisha Mwenyewe mbele yetu tena. Tulikuwa
na maombi nyumbani na wapendwa kadhaa wa kanisani na tulimlilia Mungu siku nzima.
Tuliomba hadi usiku wa manane. Dada yangu Zipporah na mimi, tulikuwa tumepiga magoti
karibu tukiomba kwa mioyo yetu yote ambapo ghafla mwanga mkubwa sana ulishuka
kutoka mbinguni. Wengi wa watu waliokuwepo chumbani waliuona. Mara mwanga huu
ukashuka na kufika pale dada yangu na mimi tulipokuwa tumepiga magoti. Ilikuwa
kama kifuniko cha kuzimu kimefunguka! Ghafla, tukasikia sauti za mayowe,
mabilioni na mabilioni ya sauti zikipiga yowe kwa uchungu! Kila aliyekuwepo
chumbani aliweza kusikia sauti. Tuliogopa kwa sababu tulijua
zilikuwa sauti za kuzimu. Sijui tulifahamuje hilo, lakini
katika ulimwengu wa roho,
unajikuta tu unaelewa mambo ambayohukuyajua…. Unashangaa tu
unayajua. Tulianza kumwomba Mungu, tukiomba rehema. Nilipofunua kinywa nilianza
kunena kwa lugha. Kisha Bwana akaanza kusema na mimi na dada yangu, akitupa
jumbe za kumpa kila mtu pale chumbani, kwa kanisa Lake na ulimwengu. Wakati
huu, mimi na dada yangu ndio tu tuliweza kusikia mayowe na maombolezo. Kulikuwa
na mabilioni na mabilioni…..wasiohesabika. Walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa.
Wengine walisikika wakilia kama wanaonyongwa. Wengine walikuwa wanapiga kelele,
“Moto!Moto!” Bwana akasema, “Wengi wa hawa watu walioko kuzimu walikuwa
Wakristo walipokuwa duniani. Waliimba, waliabudu, waliomba, lakini wakaishia kuzimu
kwa sababu hawakufanya toba ya kweli. Walienda kanisani lakini bado waliishi maisha
ya dhambi wakiwa nyumbani. Wengi wataingia mahali hapa. Ombeni rehema kwa ajili
ya ulimwengu.” Tukaanza kulilia rehema, kuombea ulimwengu, tukiomba kwa mioyo
yetu yote. Kisha Yesu akatuambia jinsi shetani alivyoweka mitego mingi ili
awanase watu waende kuzimu. Alisema, “Kuzimu haitosheki. Shetani anataka kunasa
watu wengi awezavyo waende kuzimu.”
Uchafu wa Kimapepo
Ulioenea Duniani
Yesu alituambia kuna vitu vingi vinavyotumiwa duniani ambavyo
vinatengenezwa na ufalme wa shetani kwa kusudi la kuwafanya watu wamilikiwe na kutawaliwa
na mapepo. Alituambia kuna vitu vingi ikiwa ni pamoja na vyakula, vinywaji, nguo,
(shetani amejipenyeza kila mahali. Ndiyo maana Wakristo wanatakiwa sasa kuamka
katika maombi) vyenye mapepo yaliyopewa kazi ya kumiliki watu na kuwashawishi
kutenda dhambi. Ndiyo maana ni muhimu kuombea na kukabidhi mikononi mwa Mungu
chochote tunachonunua na kuharibu nguvu za kishetani zilizokuja nacho. Alituambia
kwamba televisheni ni moja yachambo kikuu cha shetani cha kuwanasa watu waende
kuzimu. Bwana alisema, “Vipindi vinavyoonyeshwa kwenye TV havikusudii kuwaburudisha watu bali kuwapeleka kuzimu. Wengi
wako kuzimu kwa sababu ya TV. Filamu
nyingi zimeandaliwa na shetani na kuigizwa na mawakala wake ili tu kuwanasa
watu waende kuzimu. Moyo wangu unavunjika kuona jinsi wanadamu wanavyozipenda. Msiangalie
TV ya kidunia. Itawapeleka kuzimu.”
Alisema, “Ni chambo cha shetani kuwafanya mtende dhambi, kuharibu nafsi zenu.
Mnapaswa kusulibisha mwili. Msitii tamaa za mwili. Mtiini Roho Mtakatifu.”
Bwana alituonyesha mapepo yanayofanana na waigizaji wa
katuni; mengine yalifanana na katuni za Kikristo! Hili lilitushtua lakini Bwana
akatuambia sio vipindi vyote vya “Kikristo” ni vya Kikristo kweli. Vingi si vya
kweli na utambulisho wa “Kikristo” ni ili kuwanasa Wakristo waviangalie wakati
vimekusudiwa kutangaza dhambi na kupeleka watu kuzimu. Bwana alituonyesha
filamu nyingi, vitabu na hata katuni za watoto ambazo zimeandaliwana shetani na
kuletwa duniani na mawakala wake. Majina ya katuni za kimapepo na madoli (wanasesere)
ambayo alitufunulia ni Mudpit, Barbie®, Scooby Doo®, Ben 10®, Avatar, Pixel
pinkie®, na the Walt Disney® versions of Cinderella, Beauty and the Beast, na
the Little Mermaid. Bwana akasema katuni hizi zote zina mapepo yaliyopewa kazi
ya kuwatawala watoto. Yesu akaniambia, “Unaona shetani alivyo katili? Anataka kuwanasa
hata watoto waende kuzimu.” Nikaona pia pepo lililofanana na muigizaji wa katuni
ya Kikristo kuhusu Musa iliyotengenezwa na Nest Entertainment®. Pepo lilifanana
na mtoto Musa kutoka katika filamu hiyo, na lilikuwa linacheka likisema limedanganya
Wakristo! Pia niliona pepo lililofanana na Aang kutoka katuni ya Avatar! Tulikuwa
na katuni hizi nyingi nyumbani na Yesu akatuambia tuzichome. Yesu alisema,
katuni zote nilizoorodhesha hapa zimetengenezwa na sura za mapepo (yaani, kuna
mapepo yanayofanana nazo kabisa) lakini nataka kubainisha kwamba Yesu
alinionyesha baadhi tu na sio zote. Zaidi ya katuni za kimapepo nilizoona,
ambazo nimezitaja, Yesu hakunionyesha katuni zingine. Alizitaja tu akasema ni
za kimapepo. Ningependa kusema kwamba sikuona tu mapepo yanayofanana na katuni
za Barbie®, lakini niliona pia madoli ya Barbie®. Kusema kweli, niliona madoli
ya Barbie® katika maono mengi katika nyakati tofauti. Katika maono mojawapo
niliona vitu kadhaa kwa ajili ya kuuzwa stendi ikiwa ni pamoja na madoli ya Barbie®.
Moja ya hayo madoli likageuka na kunitazama na kuanza kusema kwa dhihaka kwamba
mapepo yamewadanganya wanadamu. Baadaye likasinyaa na kufanana na doli la
kawaida la plastiki! Yesu alisema hata baadhi ya vitabu vya watoto vina mapepo
maalum. Alitaja kitabu cha watoto kinachoitwa "Rattlesnake." Hatujawahi
kukiona au kukisoma hiki kitabu Yesu alichokizungumzia, lakini alisema hiki kitabu
cha watoto kinatoka kuzimu. Ndivyo ilivyo kwa baadhi ya vitabu vinavyoitwa vya Kikristo.
Yesu alitufunulia kwamba hata magazeti ya "Watchtower and Awake” yanayotolewa
na Mashahidi wa Yehova, ni ya kimapepo na hataki watoto wake wayasome. Bwana
alifunua baadhi ya magazeti ya kidunia yanayopaswa kuepukwa pia. Baadhi yao ni
magazeti ya "Drum”, “You” na
“People”. Yesu alituambia kwamba haya yote yana misheni ya kupeleka watu
kuzimu, sio kuwaburudisha. Alisema, “Dunia imekuwa mahali pa giza na ndiyo
maana nataka muongozwe na Roho katika kila jambo mnalofanya.” Alituambia, “Hivi
vitabu, filamu, drama za mvutano wa kijamii na katuni havijakusudiwa
kuwaburudisha watu bali kuwapeleka kuzimu. Ni chambo cha shetani. Msivutiwe
navyo.” Bwana alituambia shetani ameweka mapepo kwenye stika za watoto pia.
Hizi ni katuni na stika zingine kama Hannah Montana na Barbie® stickers. Alituambia
muziki wa kidunia pia utawapeleka kuzimu na kwamba nao pia ni mtego wa shetani.
Ondoeni Vitu Bandia
Alituambia hataki wanawake Wakristo wawe bandia kwa namna
yoyote. Alisema hataki watumie nywele bandia, mapambo ya vito (hereni, bangili
nk.), kope bandia, kucha bandia, rangi za kucha, rangi ya mdomo (lipstick),
wanja au vipodozi vya aina yeyote. Anataka wabaki vile walivyoumbwa. Wajivunie jinsi
alivyowaumba. Hicho ndicho kinachompendeza. Aliposema hili, kulikuwa na hasira
katika sauti Yake. Alisema, “Kwa nini mnajaribu kubadili nilichokiumba? Sitaki
vitu hivyo kwa watoto Wangu. Kama mnataka vitu hivyo, kwa nini hamtengenezi
watu wenu wenyewe ili mviweke vitu hivyo kwao. Msibadilishe nilichotengeneza!” “Vitu
hivi vyote bandia vinatoka kwa shetani. Sivitaki kwa watoto wangu.” Yesu
havitaki. Viondoeni na kutubu. Vitawapeleka kuzimu. Bwana alinionyesha kitu cha
kushtua sana; niliona pepo katika namna ya mwanamke na lilikuwa limevaa vitu
hivi vyote: kope bandia, rangi za mdomo, na nguo inayobana sana. Hapo ndipo
nikatambua vitu hivi vinatoka wapi; kwa shetani mwenyewe. Alituambia vitu hivi
vyote vimetoka kuzimu na shetani amevileta kuwadanganya watu.
Sitii chumvi katika ujumbe huu. Nasema kama Bwana alivyosema
nami. Ni jukumu langu kuwaonya kuhusu hili kwa sababu wote tutasimama mbele za
Mungu siku moja. Nawaambia ukweli. Yesu hapendi vitu hivyo. Anapendezwa
tukibaki vile alivyotuumba; hiki ndicho alichotuambia.
Staha na
Utakatifu
Alituambia hataki wanawake Wakristo kuvaa suruali au mapambo. Bwana
aliruhusu dada yangu kumsikia shetani akitoa maelekezo kwa mapepo.
Alikuwa akisema,
“Hakikisheni wanaandika 'SURUALI ZA WANAWAKE' (kwenye utambulisho [label]) ili wanawake
wazivae na kuja kuzimu.” Bwana pia alinionyesha pepo katika mfano wa mwanamke
aliye uchi, amesimama juu ya ukuta mrefu. Ingawa lilikuwa uchi kabisa na juu ya
ukuta mrefu, hili pepo liliendelea kujaribu kuuficha uchi wake kwa kufunika
sehemu sehemu kwa kutumia mikono yake na kuchuchumaa. Lakini
halikuwa limevaa nguo yoyote! Yesu akaniambia, “Hili ni pepo la utupu
linalotawala wanawake duniani na ndiyo maana wanatembea hadharani uchi na kufunika
sehemu tu za miili yao.” Yesu akaniambia tena kitu kingine. Akasema, “Hili pepo
la utupu limeingia kwenye makanisa mengi.”
Yesu aliniambia shetani anajua kwamba wanawake Wakristo wengi hawavai tena mapambo
ya vito kama bangili, hivyo amebadilisha aina ya mapambo ili kuwanasa. Sijui
kama hizi saa ziko kila mahali lakini katika nchi yangu kuna saa-bangili. Zimetengenezwa
kabisa kama bangili, lakini zina kitu kidogo katikati ambapo unaweza kuona
muda. Lakini Yesu aliniambia ni hila tu ya shetani ili wanawake waseme, “Ni saa
tu.” Pia niliona roho za nyoka kwenye hizi saa-bangili.
Alisema
anataka utakatifu kamili na lazima tuitii Biblia yote. Bwana alisema, “Fuateni
Neno
Langu.”
Pia alisema, “Dunia
imeingia katika kanisa Langu. Watu kanisani
sasa wanavaa kama watu wa duniani. Wameingiza muziki wa shetani kanisani; rock,
hip hop. Umewahi kusikia malaika wakiimba kwa kutamka (rapping)? Unaweza ku-rap
na kusema unamwimbia Mungu?” Bwana aliposema hili, kulikuwa
na hasira kwenye sauti Yake. Bwana aliruhusu pia mimi na dada yangu kuwasikia
malaika mbinguni wakitoa sifa na heshima kwa Bwana wetu. Walikuwa wanaimba, “Hosana, Hosana kwa Mungu aliye juu,” na
ilipendeza sana. Sijawahi kusikia namna hiyo duniani. Wiki chache zilizopita
Yesu aliniambia, “Waambie watu wangu, ‘Muda ni
mfupi sana na saa inafika mwisho. Usipende kubaki nitakaporudi kukusanya bibi
arusi Wangu. Mkono Wangu wa kuzuia utainuliwa na mateso yasiyoelezeka yataijia
dunia. Jiandae kwa vile kuja Kwangu ni kwa utukufu!’”
Lazima Mlinzi Awaonye
Mara ya kwanza kusikia Mungu akisema nami ilikuwa 2010.
Nilitaka sana kumsikia Mungu na nilikuwa nikimuomba aseme nami. Nilisikia sauti
ya Bwana na alisema tu “Ezekieli 33:6-7”. Nilipoisoma ilisema, “Bali mlinzi akiona
upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja
ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake,
lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo. Basi wewe, mwanadamu,
nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani
mwangu, ukawape maonyo yangu. Bwana aliponipa andiko hili, sikuelewa lina maana
gani kwangu, lakini Bwana akasema ananiandaa na dada yangu tuwe walinzi. Alisema,
“Niliwapa mstari huo kwa sababu najua kazi ninayotaka kuwatumia kuifanya. Popote
nitakapowaambia muende, mtakwenda, popote nitakapowaambia msiende, hamtakwenda.
Huu ni mwisho wa maisha yenu ya kibinafsi na kuanzia sasa mtaishi kwa ajili
Yangu. Nitawatumia kuwatoa wengi gizani na kuwaingiza nuruni. Lazima mseme ukweli
na msimuogope yeyote. Kama nawaambia mumuonye mtu fulani na hamumuonyi kwa
sababu mnaogopa, damu yao itamwagwa juu yenu. Nitawapa ujasiri na hamtashindwa.” “Wengi
watainuka kinyume chenu, hata wengi katika familia zenu watawainukia. Wengi watawapinga
na hata kutumia maandiko kuwapinga. Watawapa majina. Wengine watasema mna
mapepo lakini msivunjike moyo. Msikate tamaa kwa sababu niko pamoja
nanyi. Sitawaacha wala sitawatupa kamwe.
Lazima mseme ukweli kama ulivyo bila kumuogopa yeyote kwa sababu niko pamoja
nanyi. Wengi watawahukumu na kudhani wanamfanyia Mungu huduma, lakini lazima
muwe shujaa na hodari na kusema wazi. “Kutakuwa na mateso mengi, lakini msikate tamaa kwa sababu
thawabu yenu ni kubwa na thawabu ni kubwa kwa yeyote anayefanya kazi ya Mungu.”
Miezi kadhaa baadaye wakati mimi na dada yangu tulipokuwa tukiomba, Bwana alituonyesha
maono ya watu kwenye tamasha la muziki. Lilikuwa tamasha la muziki wa dunia na
wengi niliowaona hapo walikuwa vijana. Walikuwa wote wakifurahia lakini nilipotazama
niliona kwamba kwa juu kulikuwa na mkono mkubwa uliowafunika. Bwana
akanifunulia kwamba huu ulikuwa mkono wa shetani. Ulikuwa mkubwa sana kiasi cha
kuwafunika wote lakini walionekana kwamba hawana habari. Mkono ulitoa mafuta fulani
uliyoyaacha kwa wote walioko pale. Na Bwana akaniambia hiki ndicho kinatokea kwenye
matamasha ya muziki. Mkono wa shetani unafunika kila mtu katika matamasha haya
na kuacha kitu fulani juu yao. Pia alitupa maonyo kwa ajili ya Wakristo. “Hata
tu kusengenya kunaweza kumpeleka mtu kuzimu. Usiwaseme ndugu zako katika Bwana.
UsimseMe mtu yeyote. Jali mambo yako mwenyewe. Kama unaona mtu amekosea, sema
naye kuhusu kosa hilo na kumuombea. ”Bwana akasema, “Msifanye makosa ambayo
wengi walioko kuzimu waliyafanya ya kudharau vyombo ambavyo Mungu anavitumia
kwa sababu ya umri au
sababu nyingine yoyote. Mungu anaweza kutumia kitu chochote
na yeyote anayetaka
kumtumia.” Wiki mbili
zilizopita, nilikuwa nyumbani nikiomba. Mara nikafunga macho yangu ili kuanza
kuomba. Bwana akanionyesha shimo refu sana lenye giza. Lilikuwa refu sana, refu
kuliko kina chochote ambacho nimewahi kuona pamoja na giza nene. Nilipofungua macho
yangu sikuweza kuona kitu lakini nilipofunga macho niliweza kuliona tena. Chini
kwenye shimo hilo niliona moto wa majimaji kama unaoonekana kwenye volkano. Ulikuwa
moto mwekundu. Nilijua ni kuzimu.
Maono yakakoma. Sikia Maonyo na Ingia Kupitia Mlango Mwembamba
Siku iliyofuata usiku nilikuwa kitandani nikiongea na Yesu ambapo nikiwa
katikati ya kuamka na kuota ndoto hivi nilimuona Yesu na akaniambia anataka
kunivuta Kwake. Nikajikuta niko Kuzimu, peke yangu (Sikuona nikiwa na Yesu
Kuzimu). Palikuwa mahali penye giza sana ingawa kulikuwa na miali mingi na joto
kali. Niliweza kuhisi kuungua moto kutoka katika miali na kusikia sauti ambayo
inasikika ukiwa karibu na moto mkubwa. Kisha nikaona mtu; alikuwa uchi kabisa
na alionekana akiteseka sana. Mara nikasikia mayowe ya uchungu, “Saidia! Saidia!
Nilikuwa Muislamu duniani na sasa najuta sana. Nisaidie!” Ilikuwa
inaumiza sana kumuona huyu mtu na kusikia kilio chake kiasi kwamba nilitamani
kutoka mahali hapo. Nilijaribu kuamka lakini sikuweza. Baada yamuda nikaweza
kuamka na kujikuta nimerudi kitandani kwangu. Kwa muda niliendelea kuhisi joto
kwenye ngozi yangu, na kasha likatoweka. Baadaye nikapata maono mengine peke yangu,
sio kwa kipindi kimoja tulipata haya mafunuo niliyoyashuhudia. Nilikuwa chumbani
kwangu usiku mmoja wakati Bwana aliponionyesha sehemu ya kuzimu ya wale wanaopiga
punyeto
(wanaojichua). Hii sehemu ilikuwa inasikitisha. Niliona mwanamke
kwenye kiti. Alifungwa kwa minyororo mikubwa kwenye kiti alichokuwa amekalia na
hakuweza kusogea kabisa! Huyu mwanamke alikuwa amechomwa kiasi cha kutotambulika.
Kilichokuwa kimebaki katika mwili wake ni kama majivu. Alikuwa kijivu kabisa,
ameungua kama mkaa, na alionekana akiteseka sana. Kisha nikawezeshwa
kujuakwamba alikuwa pale kwa sababu ya kujichua katika maisha yake duniani.
Naamini Mungu alinionyesha hilo kwa sababu anataka kuwafikia waliotawaliwa na
dhambi hii. Sikiliza Neno la Mungu. Usidharau chombo chochote anachokitumia
Mungu kusema na wewe. Badala yake, tubu na kumrudia Mungu. Nakusihi sasa utubu
na kuja kwa Yesu. Usiweke imani yako kwa mtu. Weka imani yako kwa Mungu. Tubu
dhambi zako na jitahidi kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa vile wengi
watajaribu kuingia wasiweze. Yesu anatuonyesha jinsi ya kuingia lango hilo kupitia
maonyo haya anayotupa katika hizi nyakati za mwisho. “Jitahidi kuishi maisha matakatifu, kwa vile bila utakatifu hakuna mtu
atamwona Bwana.” Yesu Mwenyewe alituambia maneno haya; alisema anarudi tu kwa
ajili ya watu watakatifu. Biblia inasema usifanye moyo wako kuwa mgumu
unaposikia sauti Yake; mtafute Mungu maadamu anapatikana kwa sababu kesho
utakuwa umechelewa. Hakuna kati yetu anayejua lini tutakufa, na mara
tutakapoiacha hii dunia itakuwa haiwezekani kutoa maisha yako kwa Kristo na
kupita toka mautini kwenda uzimani. Ufu 21:8. “Bali
waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao
waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto
na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
1 Kor 6:9-11. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme
wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu
sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio,
wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa
namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika
jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”
Mungu akubariki.
Rachael Mushala
Comments
Post a Comment