Lakini
Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha;
Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu
kwa dhambi, Ataona
uzao wake, ataishi siku nyingi,
Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake (Isaya 53:10).
Roho Mtakatifu,
akinena kupitia Nabii Isaya, alitoa unabii kuhusiana
na
kuja kwake Masihi kama sadaka kwa ajili ya
dhambi na kweli kwamba Ataona “uzao” Wake, ambao utaongeza siku Zake hapa duniani. Uzao waYesu
ni Kanisa. Kupitia
Kanisa, Bwana Yesu ameongeza siku
Zake.Yesu alikuja ulimwenguni
humu, akaishi katika ulimwengu huu, akaushinda
ulimwengu, akafa, akazikwa, akafufuka, na
kupaa juu mbinguni. Lakini maisha
Yake yanaendelea leo hii hapa
duniani kupitia sisi. Sisi ndio tunaoyaishi
maisha yake hapa duniani sasa. Anaendelea kuishi, kupitia sisi (Kanisa). Matendo 1:1 inazungumza juu ya “…mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha.” Ambapo inamaanisha kazi Zake za kimiujiza na mafundisho Yake kuhusiana na Ufalme
wa Mungu. Na unavyoendelea kusoma zaidi katika Kitabu cha Matendo, utagundua kwamba Bwana Yesu aliendelea
kufundisha na kufanya mambo yale yale kupitia wale Mitume ambao alikuwa amewachagua. Wao pia (Mitume),
waliwarithisha mafundisho hayo hayo kwa wengine, na
mwishowe, imetufikia kila mmoja wetu; na itaendelea
mpaka pale Yesu atakaporudi tena. Sisi tu mabalozi Wake, tukiendelea kufundisha
mambo yale yale Aliyofundisha, na kufanya ishara
Alizozifanya.
Isaya 53:8 inasema, “…Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.”
Ulimwengu ulifikiri kwamba umemmaliza; badala yake umetokea wewe na mimi! Leo, pindi unapoenda mahali, Yesu anaonekana (anadhihirika kupitia wewe). Kila
wakati jawa na mawazo na fikra
kwamba Kristo anaishi kupitia wewe. Mtu yeyote yule anayehitaji kujua Yesu
anaonekanaje anahitaji tu kukutazama wewe! Wewe ni mng’ao wa utukufu Wake,
chapa halisi ya nafsi Yake, mshirika wa uzima Wake, na msambazaji wa pendo
Lake, haki, na neema. Wewe ni mwakilishi Wake katika ulimwengu huu sasa.
Sala
Baba Mpendwa wa mbinguni,
ninakushukuru sana kwa pendo na neema ambazo
umenikirimia. Ahsante kwa
kujidhihirisha katika ulimwengu kwa kupitia maisha yangu. Mimi ni mng’ao wa utukufu Wake, chapa halisi ya nafsi Yake na maisha yangu ni
udhihirisho wa sifa na utukufu
wa Mungu, katika Jina Lake Yesu. Amina.
Somo zaidi:
Wagalatia
3:16; Wagalatia 3:29; 2 Wakorinto 5:20
Hakika Yesu ni mwema
ReplyDelete